KAULI AMBAZO ZINAWEZA KUMUUA MWENYE MSONGO.

Maadili ambayo tunayo kama jamii,MTU akiwa kwenye kipindi kigumu anahitaji kufarijiwa.
Faraja inaweza kuwa ya aina yoyote mfano maneno ya kumfariji au hata vitu kama pesa ,nguo na zawadi nyingine. Kwanini Faraja? Faraja umfanya MTU ajione naye ni wa muhimu ,humfanya MTU ajihisi hata alichopoteza aone kipi.
MTU alikuwa na mpenz wake akamuacha anahitaji faraja,MTU aliyefukuzwa kazi anahitaji faraja,MTU aliyefiwa anahitaji faraja na mambo kama hayo.
Mfano wa faraja niliotoa ni ya maneno ,sasa kama hujui namna ya kumfariji MTU kwa maneno. Jifunze kauli ambazo hutakiwi kusema kwa mwenye huzuni.
1.Usimwambie ,kwanini anahuzunika kwani yeye siye wa kwanza. Haifai kusema hivyo.
2.Usiseme mbele yake kwamba maisha hayana huruma na MTU.Haifai acha
3.Usimwambie hati asihuzunike.No mwache kwanza
4.Usimletee kebehi eti kama ataendelea kuhuzunika itakuwa hivyo siku zote
5.Acha kumwambia alichofanya ni makosa yake
6. Usimwambie mifano yako ya kipumbavu( samahani kwa kauli hii) eti asihuzunike kwasababu ya msiba maana nawe ushawahi kufiwa na ndugu
7.Usimwambie eti akijiunga na watu yaani asikae pekee yake itamsaidia.Acha ni vibaya
8.Usimwambie eti jinsi alivyo anamfanya kila MTU ahuzunike.Mwache kama huna la kusema
9.Usimuulize eti umpe kinywaji .No mwache atulie.
Nadhani kauli zetu tutaziacha na kuangalia namna nzuri ya kuwafariji wenzetu.

Asante kwa mara nyingine tena ,usisite kutembelea ukurasa huu kila mara.

Comments