KWANINI HUWA TUNASEMA HAKUNA KUKATA TAMAA?

  Masomo haya ya saikolojia yanaendelea.Leo naendelea na suala la KUKATA TAMAA.
Tuliangalia Sababu ambazo huwa zinasababisha watu wengi KUKATA TAMAA mara nyingi, sasa leo ni vema kujiuliza ili swali KWANINI HAKUNA KUKATA TAMAA? AU KWA NAMNA NYINGINE HIVI KWANINI UKATE TAMAA?
Sababu za suala hili nahitaji kuanzia leo zikupe motisha mpya ya kutokata tamaa .No matter what you have to move forward.Sababu hizi ziwe hamasa narudia tena;-
1.Usikate tamaa maana hujafanya au haujajaribu kila kitu au MTU.Nikutie moyo maana huenda ulikuwa mfanyabiashara wa mazao lakini leo umefirisika,jaribu kwingine usichoke.

2.Kama hujui MAFANIKIO yapo mlangoni.Yaani siku ambayo unaona kila kitu hakiendi ndio huwa umekaribia kilele cha MAFANIKIO. Yeyote aliepo kwenye usafiri hasa wa Maji anajua, meli ikikaribia kutia nanga lazima chombo kiwe na msukasuko.
3.Usikate TAMAA maana hapo ulipofikia ukipaacha tu mwenzako atapamalizia nawe utabaki kujilaumu.Mifano kama hii unaiona kwenye ndoa, wewe unatoka mwenzio anaingia na maisha yanaendelea.Maisha ni safari kama hujafika hakuna kushuka njiani.

4.Hutakiwi KUKATA TAMAA maana palipo na MAFANIKIO hapo pia kuna vikwazo vingi lakini pasipo na MAFANIKIO njia ni nyeupe.Waendao uzimani njia yao ni nyembamba na imesongwa lakini njia ya upotevuni ni pana na safi kupita 
5.KUKATA TAMAA  ni kwamba umepata lakini kama hujapata bado lazima mapambano yaendelee

6.Ni bora ufe ukiwa unajaribu kuliko kufa ushajikatia tamaa.Askari shujaa ni yule anaefia vitani
7.Usikatishwe TAMAA na mambo yaliyopita maana hayo hayawezi kuharibu maisha yako ya mbeleni. Waswahili huwa wanasema"yaliyopita si ndwele tugange yajayo"

8.Kama huko hai kila kitu kinawezekana ,hakuna KUKATA TAMAA.

Nitaendelea na masomo haya ya saikolojia kwa mada kede kede ,usisite kutembelea blog hii.
#bless

Comments