KWANINI WENGINE HUFANIKIWA NA WENGINE HUSHINDWA?

Hili ni suala ambalo na wewe unaweza kujiuliza .Hivi ni kwanini Mimi sifanikiwi na wengine wanafanikiwa?
Ni suala mtambuka yaani kila siku lipo lakini ili kuelewa mantiki nzima ni bora tuelewe "kufanikiwa" ni nini? MAFANIKIO(BREAKTHROUGHS) ni nomino ila kitenzi chake ni kufanikiwa .
Kufanikiwa ni sawa na kusema "kufa"+" kuwa" au kwa kimombo ni "die+to be". Wewe ulipo ni mbegu na mbegu ili izae inatakiwa kufa ili izae kiumbe kipya au matunda zaidi. Mfano Mbegu ya haragwe huwa ina " break" halafu INA through (pita) mche mpya Wa haragwe.Hii ndio maana ya "kufanikiwa".

Baada ya kuona maana ni vizuri kujikita kwenye mada husika maana ukielewa maana ya kitu umeelewa maisha.KWANINI WENGINE WANAFANIKIWA NA WENGINE HAWAFANIKIWI?
Mambo yanayoweza kufanya MTU afanikiwe ni pamoja na
1.Misingi ya wazazi au walezi.Moja ya msingi wa maisha ya baadaye ya mtoto huanza na wazazi au walezi.Hawa ndio watakuwekea msingi wa maadili,elimu, talanta na mambo kama hayo.Bahati mbaya wengi huwa wanakosa hapa na Wakati mwingine wazazi wanaweza kuwa na Mali lakini wakashindwa kukuingiza kwenye mfumo moja kwa moja.Mfano mzuri utasikia baba akisema'hizi ni Mali zangu na mama yenu na nyie tafuteni za kwenu" ni makosa mzazi kusema hivi.Tujifunze kwa Waarabu na wazungu,ambao wao wana mtindo wa kuendeleza Mali zao vizazi na vizazi na kwenye dunia hii nduo watu ambao hawana Shida za umaskini.
2.Kulipa gharama. Hapa gharama zinaweza kuwa ada za masomo au wewe kujitoa kisawasawa.Tulio wengi tunaogopa kuwekeza yaani tatizo alilonalo MTU maskini ni kuwekeza.Tajiri huwekeza lakini maskini yeye anapenda kutunza alicho nacho.Kwahio basi uwekezaji ndio huleta MAFANIKIO kuliko huifadhi wa ma mali.Uwekezaji sio pesa tu inaweza kuwa taaluma,muda,fedha au hata watoto wako.
3.Kuiishi kalama yako.Wengi huishi bila kujua wafanye nini ? Leo kacheza mpira kesho kaimba keshokutwa kaigiza mtondogoo kawa Fundi simu.Hata malaika wa riziki akija hawezi kuelewa unafanya nini? Kiukweli ukijua karama yako na kuitendea kazi utaona wepesi tu.Swali lako itakuwa ni je nitajuaje kalama yangu? Muulize mzazi au mlezi wako, he ulipokuwa Mtoto ulikuwa unafanya nini atakachokwambia ndicho kipawa chako maana asili ya maisha huanza udogoni.Mfano MTU ambaye hakucheza michezo ya baba na mama, huyo ni ngumu kuwa na familia.
4.Matumizi ya muda.Muda ni Mali na sio uongo.Ebu jiulize kwanini unalipa Tsh 50000 kwenda Mwanza kwenye basi Wakati miguu ya kutembea kutoka Dar mpaka Mwanza unayo? Si kwamba huwezi kutembea ila unakuwa unanunua muda.Safari ya kutembea miezi 2 unaifanya siku moja.Sasa je muda wako wa kila siku unautumiaje? Dangote pamoja ni kwamba ni tajiri bilionea yeye hutumia masaa 4 kulala na 20 huwa anafanya kazi.Kaka yangu Mzee Strive Masiyiwa ,yeye anasema masaa 18 yote uyatumia kwa dili zake za pesa ingawa ni miongoni mwa watu 10 wenye ngozi nyeusi matacoon.Je wewe unashinda na smartphone ukimfatilia Wema,Zari na Diamond ambao hata hawakufahamu ni wewe basi?
5."Busy for nothing ".Hapa ni kitendawili,MTU unakuwa kama sisimizi maana utafiti unasema kati ya viumbe wote dunia hii kiumbe sisimizi ndio huwa halali tangu anatoka kwenye yai.Yeye na kazi ,kazi na yeye.Unaweza kuwa wewe au Mimi.MTU unafanya kazi kila siku lakini kula kwa Shida, kuvaa Shida, watoto kusoma ni Shida tupu.Jiulize kazi unayoifanya inakulipa? Unaweza kuwa Mwalimu,Daktari, Mhasibu na kazi unafanya lakini MAFANIKIO hakuna, wewe ni wa madeni tu ukipata mshahara wote unampelekea Mpemba dukani kama bill ya deni lake ili mwezi unaoanza uanze kukopa upya.Chonde hii sio kazi ni kibarua heri uache tu au ubadili matumizi.
6.Wanaofanikiwa ni wale wanaochagua njia moja na kuifanya kwa usahihi.Huenda una kazi na unajiona una vipaji vingi lakini Hii haitakusaidia kama hutashindwa kujikita sehemu moja.Mfano mzuri ni kwa wacheza mpira ,ukiwa kiraka yaani leo umecheza namba 4 kesho 7 keshokutwa 11 yaani namba yako haieleweki siku akija anaecheza namba io wewe hutopata namba maana hueleweki.Chagua njia moja itakufanikisha maana duniani si kujua vingi Bali vichache vyenye manufaa.

Asante kwa muda wako usisite kuitembelea blog hii kila mara.

Comments