Kuishi kuna mambo mawili makuu nayo ni mambo mazuri na mabaya.Kila MTU huwa anapenda mambo yake yote yawe mazuri na hakuna anaependa mambo mabaya.
Pamoja na kutamani mambo mazuri na kuiweka akili kupenda mambo mazuri ndio huwa kuna zaliwa kitu kinaitwa KUKATA TAMAA.
KUKATA TAMAA huwa kuna tokana na kuangalia upande mmoja wa shilingi,kupata tu Kukosa no.Sasa Kutokana na Mimi mwenyewe na kwa kuangalia jinsi mambo yalivyo nimetoa orodha ya sababu ambazo hufanya wengi wetu KUKATA TAMAA. Lengo ni wewe na mimi kuelewa chanzo na ukifahamu chanzo cha tatizo ni rahisi kutafuta suluhisho.Sababu ni kama zifuatazo:-
1.Wengi huwa tunapenda kufanikiwa haraka yaani hatuna uvumilivu na kujipa muda.
2.Huwa hatujiamini au hatuamini tunachofanya
3.Wengi wetu tumekuwa na kasumba ya kutoachilia yaliyotukwaza .Mfano mpenz wako alikuacha Wakati unampenda,unaona wote wanaokwambia wanakupenda wako kama aliyekuacha.
4.Tunaishi kwenye makosa au tunarudia makosa yaleyale kila siku.
5.Tuna Woga wa mambo ya mbeleni yaani tunasema kesho itakuaje?
6.Wengi huwa hatupendi kubadilika. Unajua kilichokufanya ufukuzwe kazi ni pombe lakini hutaki kuacha.
7.Wengi wetu hatuamini kwamba tunaweza pekee yetu mpaka tuwezeshwe ,mwisho wa siku wanaotuwezesha wanatuchagulia jinsi ya kuishi na kufanya kipi ambayo si matarajio yetu.
8.Tunaamini sisi ni wadhaifu.Yaani boss wako unaona anachokwambia ni tofauti na career yako lakini huwezi kujilinda,unakubali ili ulinde ugali.
9.Wengi tunadhani dunia hii sisi ndiowenye mikosi.
10.Wengi tunahofu ya kwamba tutashindwa tu kila tulifanyalo badala ya kutamani kuona tunachofanya kitafanikiwa.
11.Wengi hatuna maono ya kuangalia yanayowezekana badala yake tunaforce mambo
12.Tunaamini au tunahisi mambo fulani sisi hatuyawezi au yanastahili kufanywa na WENGINE wala si sisi .Umejaribu ukashindwa ndugu yangu?
13.Kufanya kazi kupitiliza. Yaani unafanya kazi ukiwa na matumaini unatoka.kufanya kazi sio tatizo ,tatizo ni je kazi unayoifanya inakulipa au inakidhi mahitaji na akiba juu?
14.Wengi Tunaamini Shida zetu wengine hawana.Waswahili wanasema"MTU na lake moyoni "
15.Wengi wetu tunaamini kushindwa kwa siku moja ndio kila siku itakuwa hivyo.
16.Wengi hupenda kusikitika na kujutia walio yafanya.Kubali acha maisha yaendelee.
Yote Tisa ,kumi KUKATA TAMAA ni dhambi.
Nashukru kwa muda wako ,tembelea hapa Kadri huwezavyo kupata mambo mapya.
Pamoja na kutamani mambo mazuri na kuiweka akili kupenda mambo mazuri ndio huwa kuna zaliwa kitu kinaitwa KUKATA TAMAA.
KUKATA TAMAA huwa kuna tokana na kuangalia upande mmoja wa shilingi,kupata tu Kukosa no.Sasa Kutokana na Mimi mwenyewe na kwa kuangalia jinsi mambo yalivyo nimetoa orodha ya sababu ambazo hufanya wengi wetu KUKATA TAMAA. Lengo ni wewe na mimi kuelewa chanzo na ukifahamu chanzo cha tatizo ni rahisi kutafuta suluhisho.Sababu ni kama zifuatazo:-

Comments
Post a Comment