HATUA ZA KUJIFUNGUA.
1.Hatua ya utungu wa kuzaa
2.Hatua ya kuzaa mtoto
3.Hatua ya kuzaa kondo
- Sasa hili somo lieleweke vizuri ni vema twende hatua Kwa hatua. Usisahau kusubscribe channel hii.
HATUA YA UTUNGU WA KUZAA .
Hii ni hatua yenye Vipindi vitatu;vipindi hivi ni Uchungu wa awali,Uchungu shamivu na uchungu wa mpito.
A)Uchungu wa awali ni matokeo ya mlango wa kizazi kusinyaa na kupanuka mpaka centimeta 3.
B)Kipindi cha pili ni cha uchungu shamivu/shamili ambapo mlango wa kizazi huwa unatanuka mpaka sentimita 7
C)Kipindi cha tatu cha uchungu ni cha mpito ambacho mlango wa uzazi huwa unatanuka mpaka mwisho yaani sentimita 10.
Yote haya huwa yanatokea bila mwanamke kuona mikunjo io Bali hisia za utungu tu.
Wengi wa wanawake huwa wanaona Maumivu ya mgongo,Tumbo kujaa ,kuarisha,damu kutoka ukeni hasa mfuko wa Maji ukipasuka .Pia huwa kuna hisia Fulani Wakati wa Utungu kama Mshangao wa kinachoendelea,Matarajio ya kiumbe kipya ,woga,Wasiwasi lakini kuna baadhi ya hakina mama huwa wako kawaida.
- Hali ikiwa hivi maana sio dalili zote utazipitia,inaweza Kuwa moja au mbili lakini sio zote. Ukipatia hali hii ya uchungu Fanya yafuatayo;-
- Kuwa na utulivu.Mhudumu tayari anakuwa ashakwambia ni wakati upi sahihi unatakiwa kuongea nae.Sio kila uchungu ni dalili ya kuzaa,uchungu wa kipindi shamivu ndio unaweza kumuita au kama unatokwa na majimaji yenye ukijani au damu kutoka ukeni.Wakati mwingine muite kama hausikii dalili za mtoto kicheza tumboni ingawa ni ngumu kutambua hasa wa uzazi wa kwanza.
- Wakati wa usiku ni vema kulala usingizi.Kwenye kipindi cha awali cha uchungu chukua hatua ya kulala maana kuna hatua za mbeleni utashindwa kulala. Kama utakuwa na usumbufu wa kinakufanya tumboni usilale kitandani maana utaona uchungu hauishi.Cha kufanya kama huko hospital, tembelea wodi za wazazi au kama huko nyumbani andaa mashuka na mambo yote anayohitaji mzazi tiyari kwa kwenda hospital.
- Wakati wa mchana Kama unahisi uchungu, Fanya mizunguko usipende kukaa sehemu moja hata Kama ulikuwa huna cha kufanya. Na Wakati unafanya hivyo, Fanya mawasiliano na MTU atakaekupeleka hospital au mkunga na kama huwezi kupiga simu omba kusaidiwa.
- Jitayarishe sasa muda wote.Oga Maji ya moto hasa kama chupa ya Maji imepasuka.
- Kula chakula kama una njaa.Kula matunda au chochote ulichoelekezwa na Mhudumu wako.Usile kushiba sana na Epuka kula nyama na vyakula vya mafuta .Hakuna Mhudumu anaeshauri kula kupitiliza kipindi cha utungu na Epuka kunywa juisi zenye ukakasi kama machungwa au ubuyu.
- Kumbuka kukojoa mara kwa mara hata Kama haujahisi Mkojo mwingi.Mkojo mwingi kwenye kibofu huwa unaongeza uchungu.
Somo ili ni endelevu.
Asante kwa muda wako tembelea blogspot hii kila Mara.
#bless
Thank you. Nimejifunza kitu
ReplyDeleteAsante sana nmejifunza kitu
ReplyDeleteOk thanks am moted
ReplyDelete