HIVI NI KWANINI KILA MTU HUWA NA MATARAJIO NA KESHO?

  ...#Tangu nizaliwe huwa nasikia kila MTU anaitamani kesho. Kesho nitafanya hivi,kesho nitaenda kule na mambo kama hayo lakini kesho kimekuwa ni kitendawili maana haijulikani.Swali huwa ni je nani kaiona kesho?
   Katika kujadili ili swali ni bora tutazame Sababu za matamanio ya kesho ndio muktadha wa kuiona kesho utaeleweka.Kesho inabeba malengo yetu mengi,sasa ebu tuangalie sababu ambazo hubeba kesho .
.Kila kizazi kinachozaliwa ni bora ya kilichopita.Ili halina mjadala,wazazi wetu wanaona maisha yetu Leo ni bora zaidi yao.Vipo viashiria vya ubora huu kama sayansi na teknolojia.
.Watu wenye weledi(warujuaji) huitazama kesho tu.Kesho hupangwa Leo kwahio basi watu wengi wenye pesa,elimu huwa wanawekeza zaidi kwaajili ya kesho

  • 3.Kadri tunavyo sogea mbele teknolojia imekuwa na pia inatupa kitu cha pili ambacho ni ufafanuzi.Teknolojia ya leo inafanya mpaka hutamani kuona ni nini kesho kitakuepo? Wakati kuna simu za windows, tuliona simu hizo ndio bora lakini kuna iOS na android ambazo nazo najua zishapitwa na Wakati ambapo kuna maingizo mapya.Yaani lazima huitamani kesho tu.
  • Kuna ukwasi mwingi kuliko kipindi chote.Yaani hakuna utajiri ambao upo kama wa kila iitwayo Leo.Mambo yanarahisishwa na wakwasi wanakuwa wengi kila siku.
  • Jamani unajua kila siku zinavyosonga mbele wanawake wanapendeza! Kila siku wanawake wazuri wanazaliwa,wanawake wanajipendezesha na kupendeza yaani unatamani kesho uwepo uone picha mpya.
  • Kadri siku zinavyoenda mbele kuanzisha biashara ni sawa na bure.Unajua ni kwanini? Ebu vuta picha eneo ulilopo kama barabara,daraja au mnara wa simu usingekuepo biashara unayoifanya ingegharimu mtaji bei gani kufungua biashara? Leo hii na kesho biashara zinafunguliwa kwenye simu na vifaa vingine vya kidigital kwa mtaji MDOGO na kuingiza faida nyingi.Ndio maana kila MTU anaitamani kesho.
  • Maajabu ya kesho kwenye suala la mawasiliano lina maajabu makubwa.Leo hii dunia ina watu zaidi ya 7.8 billion lakini wanaotumia mawasiliano ni zaidi ya 4 billion. Kati yao watu 2 billion unaweza kuwasiliana nao bila Shida. Najiuliza hii ni Leo je kesho itakuaje? Yajayo yanafurahisha na kushangaza.
  • Wengi wa watu wanafanya shughuli zao wakiwa nyumbani. Tunaitamani kesho maana INA mambo mazuri na ya kushangaza.Nakumbuka miaka ya nyuma, wazee wetu walitumia nguvu nyingi sana hasa kwenye kilimo.MTU analima hectare 1 kwa mwezi lakini Leo kulima hekari ni nusu saa ,pia watu wa kipindi cha nyuma waliamini ili kuvuna sana inatakiwa ulime eneo kubwa. Leo hayo mambo hayapo yaani ndani ya eneo la mita kumi unaweza kuvuna maradufu.je kesho itakuaje, lazima tutamani kesho tuwepo tuone kitakachojiri .
  • Kuishi kumeongeza kuliko kipindi cha nyuma. Umri wa watu kuishi unaongezeka kila siku Kutokana na mambo mbalimbali kuzingatiwa.Afya:wazee wanatibiwa bure au bima,Chanjo kwa watoto juu ya magonjwa nyemelezi.Miundombinu: nyuma watu walitembea na kupoteza nguvu nyingi Kutokana na ukosefu wa barabara safi,magari,ndege pia WENGINE walipoteza maisha kwa kuliwa na wanyama wakali.Je kesho itakuaje iwapo mapungufu yaliyopo sasa yakifanyiwa marekebisho na maboresho? Hakika itapendeza tu .
Shukrani kwa muda wako ,usisite kutembelea blog hii kila mara kupata habari na ufahamu kede kede.
#bless

Comments