Pichani ni daktari wa masuala ya hakina mama na watoto hasa uzazi na malezi.Dada huyu ana miaka 28 ingawa yeye anaishi code namba moja yaani USA.Kwanini nimemtaja Dada Mirena?
Kwetu huku kupata udaktari katika miaka hii ni NDOTO Kutokana na mazingira yetu.Mazingira yanatukwamisha lakini sio mazingira yote yanatukwamisha,siye pia huwa tunaruhusu kukwama.Sasa Leo nakupa mambo 10 ya kufanya ili utengeneze upekee au uwe wa kipekee.Mambo haya ni:-
1.Jiepushe na matukio yasiyo na msingi au faida kwako.
2.Achana na mambo ambayo huna uwezo nayo fuata tu ambayo unayaweza.
3.Acha kujifananisha na WENGINE maana wewe ni wewe na WENGINE ni WENGINE
4.Kuwa na imani kubwa kuliko woga kwa kila unachotarajia au unachofanya
5.Epuka kujihusisha na jambo lolote ambalo halifai
6.Tumia muda japo MDOGO mara moja moja pekee yako .Jitafakari mwenyewe.
7.Usipende kuomba msamaha kwa WENGINE bila kuanzia kwako
8.Jiongeleshe kwa upole na pia Fanya hivyo Kwa WENGINE
9.Usipende Kuwa na watu ambao ni kupe kwako, kaa nao mbali.
10.Achana na maamuzi yasiyofaa.
Kidogo kidogo ukifanya siku moja utakuta umebadilika.
Asante kwa muda wako na pia usisite kutembelea blog hii upate maarifa kede kede.
#bless
Comments
Post a Comment