#Wengi wetu tukipatwa na jambo huwa tunajutia na hata kuharibu utu wetu.Ili ujue thamani yako ni vizuri kutumia muda mwingi kujifunza habari za saikolojia ili ujifahamu zaidi. Kwanini unatakiwa kujijua na kujitambua? Ni kwasababu hutakuwa na majibu sahihi juu yako na hutoenda kwa hulka kama walivyo wanyama. Mfano, Leo hii MTU anakuita "wewe ni Malaya" unaruka unamtukana au kumpiga.Hapana utakiwi kuwa wa hivyo,wewe unatakiwa kwenda maili elfu kujiuliza kwanini huonekane hivyo na Wakati wewe hufanyi hivyo;ndio maana ya utu na si uanadamu.
Sasa tujikite kwenye swala letu juu ya majuto au kujilaumu mwenyewe.Jifunze mambo haya 10 ambayo hutakiwi kuyajutia.
Kumpenda MTU.Ina maana sana kupenda na kupendwa lakini kupenda ni bora zaidi kuliko kupendwa.Ukitafuta kupendwa utachoka maana utatafuta au itakulazimu kutafuta namna ya kupendwa, wanaotafuta kupendwa huwa wanachoka haraka kuliko wanaopenda.Usijiulize kupenda, penda tu wala usijute.
Sema "sitaki " au "hapana". Kuwa muwazi katika maamuzi yako yaani ukisema hapana iwe hivyo. Kuna watu hawana msimamo,Leo akisema hapana kesho anasema ndio kwa jambo ilo ilo hata kwa MTU yule yule.Jifunze kusema hapana na usijutie kusema hapana, itakusaidia.
Ishi NDOTO yako.Kuishi NDOTO ni jambo binafsi ,kama una NDOTO hata ya Kuwa mvuvi wa samaki,kuuza Maji ya kwenye mfuko, Mwalimu au askari ishi tu hivyo ina maana. Kuna watu wengi walikuwa na NDOTO Fulani lakini wameziacha kwa Sababu ya watu Fulani.Ishi NDOTO yako na usijute kwasababu ya NDOTO io,Panga na chagua uishi pia.
Vipaumbele.Vipaumbele na malengo ni vitu ambavyo haviachani au kuvitenganisha.Weka vipaumbele na viamini usije kuvijutia.Umeweka kipaumbele ni kuoa,ni vyema oa acha mengine. Usijute au kujiuliza sana.
Achana na mapenzi sumu.Hapo juu nimesema juu ya kumpenda MTU ni vizuri lakini lazima vigezo na masharti vizingatiwe.Usijilazimishe kupenda au kupenda kupendwa kwa lazima. Kama tayari ushatengeneza UFA huu usijilaumu songa mbele kama huwezi kuacha.Kama unaweza kuacha ni vizuri sana ili usiendelee kujilaumu na kujuta.
Kusema ukweli. Kiukweli watu wengi hawapendi au hawawezi kusema ukweli. Usijilaumu kwa kusema ukweli, ukisema ukweli ni rahisi kuuishi lakini uongo utakufanya ukosehe kwenye baadhi ya mambo. Unasema una pesa nyingi lakini hata kuvaa,kula,na kulala kwa SHIDA.Sema sina huenda ukasaidiwa.
Tenga muda wako.Matumizi ya muda ni wewe kuyapanga na ukipanga muda wako utumie.Hata kama muda wako ni wa kuangalia TV ni vema na si kwamba unapoteza muda.Usijilaumu juu ya muda;WENGINE hujilaumu kwa kusema nimepoteza muda katika masomo nilitakiwa nitafute pesa, hapana uo ni muda wako usijute.je ukijuta ni nini utapata kama sio kujiumiza?
Kuchelewa juu ya mambo mbalimbali. Sawa umechelewa kuzaa au kula sasa unajilaumu nini kwani kuna aliekuzuia kufanya hivyo? Usijilaumu! Lawama ni kutokubali matokeo.Hata kama umechelewa kubali na endelea mbele ili maisha yaendelee.
Usijilaumu juu ya mapungufu yako.Kubali kwamba wewe ni mlemavu au una sura isiyo na mvuto.Kubali huna chochote, Kubali wewe ni yatima,Kubali shuleni ulisoma lakini hukuweza kukariri vizuri. Kubali mapungufu yako itakusaidia kuona pahali pa kuanzia .
Je umepata chochote kipya? Usisite kutembelea blog hii kila mara kwa maarifa kede kede.
Comments
Post a Comment