Ndoto inaweza kutafisiriwa kutokana na muktadha wake.NDOTO huwa zinazalishwa ndani ya Ubongo Kutokana na mazingira ya nje.NDOTO hizi huwa zinatengenezwa kwenye Ubongo wakati unafahamu au haufahamu;zile ambazo unafahamu ni zile ambazo zimefanyika katika maono yako na matendo yako na hizi ndio NDOTO za watu wengi. Zile NDOTO ambazo huwa unaota bila kufahamu zinatokana na Wakati umelala na fahamu ya kwamba hata ukilala Ubongo huwa unaendelea kufanya kazi.Pia zipo NDOTO za "Kuwa" Mfano Nina NDOTO ya kuwa Mhasibu,Daktari au Mchungaji nazo ni NDOTO, ndio maana NDOTO unaweza kuitafisiri Kwa muktadha wake.
Tujikite kwenye mada yetu,juu ya kwanini wanawake wengi huwa wanaota wanabakwa?
-----------------------------------------
Utafiti unasema kwamba theluthi moja(1/3) mpaka theluthi mbili (2/3) ya wanawake huwa wanaota wakilazimishwa kufanya mapenzi.
------++----------
Wanawake kati ya asilimia 33 huwa wanaota NDOTO hii kwa mwaka, asilimia 26 mara chache huwa wanaota NDOTO hii Kwa mwaka, asilimia 20 mara moja walau kwa mwezi na asilimia 21 huwa wanaota NDOTO hii kila Juma au zaidi. Wewe sijui huko wapi hapa?
Sasa Kwa hili hakuna uchunguzi wa kimahabara umefanyika,sana sana kuna Dhana au nadharia ya kwanini hii ndio NDOTO ya wanawake?
----------------
Dhana hizi ni Kama zifuatazo:
1.TAHADHARI YA KUEPUKA KUBAKWA.
Nadharia hii inatokana na woga,Wasiwasi au hata aibu ambayo ataipata msichana endapo atabakwa.Dhana hii umpelekea kuwa na mawazo ya hayo muda wote na Kadri anavyowaza hivyo ndivyo Ubongo unarekodi fikra hizo.Usiku akilala mawazo Yale yanakuja yakiwa katika hali ya video ndio NDOTO io.
2.TAMAA YA KUPENDA NGONO.
Mniwie radhi ili ni darasa kwahio unatakiwa kuongea vitu halisi.Dhana hii ni kwamba wanawake huwa wanaota NDOTO za namna hii Kutokana na MATAMANIO yao kwenye Ngono. Kama ni wewe basi utajua la kufanya.
3.Mwenendo juu Ngono.
Hapa sio tamaa bali namna unavyoishi .Mwanamke ambaye hana woga au hana aibu na masuala ya Ngono au ni mpenzi wa kutazama picha na video za ngono nae ni miongoni mwa watu watakuwa na NDOTO za namna hii mara kwa mara.
-------------------
Sasa kuna MTU atasema nifanye nini sasa? Fanya kinyume na dhana hizo.
Asante kwa muda wako pia usisite kutembelea blog hii Kila mara.
#ElimuAkili
#bless
Comments
Post a Comment