Mwanadamu na MTU ni tofauti. Mwanadamu ni mwili Wakati MTU ni roho .MTU ndio huongoza mwanadamu kwahio basi ukimfahamu MTU basi na mwanadamu atafahamika.
Kumbuka,ili kujifunza juu ya MTU na mwanadamu ni haraka iwapo Wewe mwenyewe utajijua.Sasa ebu tuangalie mambo ambayo watu wanayo na huwa yana maana gani au yanaashiria nini?
Kumbuka,ili kujifunza juu ya MTU na mwanadamu ni haraka iwapo Wewe mwenyewe utajijua.Sasa ebu tuangalie mambo ambayo watu wanayo na huwa yana maana gani au yanaashiria nini?
1.Watu ambao hupenda kuwafurahisha WENGINE wao hubaki katika hali ya upweke
2.Watu wenye aibu huwa wanaongea kidogo mambo yao lakini huwa yanawafanya WENGINE kuona wamewafahamu zaidi
3.Watu wenye akili ni wepesi wa kufahamu mawazo na hisia za WENGINE
4.Watu ambao wanapenda kushauri sana WENGINE wana matatizo zaidi ya wale wanaowashauri
5.MTU nadhifu ni mwepesi kuwaza na pia ni mwepesi hata katika kuandika
6.Watu huwa wanavuta hisia za WENGINE wanapozungumza mambo ambayo waliwahi kuyapitia
7.Watu wawili wanapokuwa wanazungumza wamesimama,mmoja kati yao akianza kuongea huku anatembea huwa anaashiria kutaka kuondoka au hajakubaliana na mwenzie anachosema
8.Watu wanaongea lugha tofauti huwa wanahamisha utu wao wanapoongea lugha moja na kuamia nyingine. Mfano MTU akizungumza kiswahili utamuona mswahili hata kama ni mzungu.
9.Watu wenye akili sana wana marafiki wachache ukilinganisha na watu wa kawaida, wenye akili hupenda Kuchagua.
10.Asilimia 90 ya meseji wanazotuma watu kwa WENGINE, maneno Yale hawawezi kuyasema mbele ya waliowatumia hizo meseji.
11.Watu wanaopenda kuongea kwa kuapa ni kwamba wana hisia Kali au muhemko
12.Watu wanaolalia mito mingi kitandani ni wapweke na wenye sonona
13.Watu wanaoandika malengo yao wana huwezekano wa asilimia 42 kufanikiwa kuyatimiza
14.Watu wanaokasirika hata kwa mambo ya kijinga ,bila kufahamu wanahitaji au wanatamani kupendwa.
Kwa Leo ngoja tufungie hapa.
Asante kwa muda wako,nakusihi sana usisite kutembelea blog hii kila mara upate maarifa kede kede.
#bless

Comments
Post a Comment