ZIFAHAMU RANGI ZINAZOVALIWA ZINA WAKILISHA NINI?

Kabla ya yote ningependa kusema ya kwamba rangi ni zile ambazo huonekana kwenye Upinde wa mvua tu.Hizo ndio rangi mama.
Sasa tujikite kwenye mada husika,rangi zinazovaliwa huwa zinawakilisha nini? Kwa mfano wapenda soka Klabu kama ya Chelsea hutumia Uzi wa bluu,Manchester united hutumia Uzi mwekundu nk Je huwa zina maanisha nini? Fuatilia
1. Rangi Nyekundu.
Rangi huwakilisha  HAMASA,UPENDO, UWEZO, NGUVU/MAMLAKA na MATAMANIO. Ngoja nigusie kidogo, mfano marais huwa wanavaa Neck Tie nyekundu kuwakilisha au kuonyesha mamlaka waliyo nayo.
2.Rangi ya Bluu
Rangi hii huwakilisha TUMAINI,USHINDANI,AMANI,UAMINIFU,AKILI
3.Rangi ya Njano
Rangi hii huwakilisha FURAHA, NGUVU,UBUNIFU,MAJIRA/NYAKATI NZURI na SHANGWE
4.Rangi ya Kijani kibichi(Green)
Rangi hii huwa inawakilisha UBORA,ASILI,UPONYAJI,UKUAJI/MAKUZI na UPYA
5.Rangi ya Machungwa
Rangi hii huwakilisha KUJIAMINI,MAFANIKIO, UHODARI,URAFIKI na UJAMAA/UNDUGU
6.Rangi ya Pinki
Rangi hii huwa inawakilisha UNYOFU,YA KUCHEZEA,UTAMU,MAWASILIANO na UPYA
7.Rangi ya Zambarau
Rangi hii huwakilisha MATAMANIO, MAMBO YA KIROHO,UKWELI, ANASA na IMANI
8.Rangi ya Weusi
Rangi hii huwakilisha MAIGIZO yaani vitu visivyo vya kumaanisha,ULINZI/KUJIHAMI,HUZUNI,UTARATIBU/DESTURI
9.Rangi ya Kahawia (brown)
Rangi hii huwakilisha URAFIKI,MAISHA MAREFU,MAMBO YASIYO SAWA,UWAZI

Natumaini umeelewa maana ya Rangi huwakilisha nini kwahio hutopata tabu kwenda msibani ukakuta watu wamevaa nguo nyeusi  
#ElimuAkili
Asante na usisite kutembelea blog hii Kila Mara upatapo muda.
#bless

Comments