IMANI YA KIKATOLIKI NA MTAZAMO WA WANAZUONI

KanisaKatoliki ni miongoni mwa makanisa mama ya kile kiitwacho Ukiristo.Kama linavyojulikana na wengi ambao ni waamini na wasio waamini wake ,Catholic "katholikos" kwa kigiriki humaanisha "universal' kwa kingereza na kwa kiswahili ni" ya wote au ya ulimwengu".
Kanisa Katoliki ambalo lilichukua imani ya kiniseni(Nicene Creed) ambayo huamini katika MUNGU mmoja na nafsi tatu yaani Mungu baba,mwana na roho mtakatifu.Kwa mujibu wa historia za Warumi ambao walitawala dunia kipindi cha Kaisari baada ya kuupiga utawala wa Umedi na Uajemi.Warumi waliamua kuja na mpango mpya wa kujiingiza katika masuala mazima ya dini.


HISTORIA YA KANISA
Ukatoliki ulianza zama za Theodoris mnamo mwaka wa 110 baada ya kifo cha Yesu Kristo. Kama ilivyokuwa falsafa ya mtawala mpya alietaka kuondoa nakama za utawala wa kimabavu ambao ulikuwa tishio kwa wengi,THEODORE alitafuta mbinu mpya ya kujipatia umaarufu na kuweza pia kutuliza vuguvugu lilikowa limeanzishwa na Yesu Kristo na wanafunzi wake.Vuguvugu la neno la MUNGU lilikuwa tishio kwa mfalme.

MFUMO WA UTAWALA
Kanisa Katoliki lipo chini ya Papa ambaye ndio hutajwa kuwa mrithi wa Petro mwanafunzi wa Yesu.Papa uchaguliwa na kikao cha makadinali cha siri(Papal conclave). Utaratibu huu wa kumchagua Papa yaani PAPABILI kwa kiitaliano ,ulianza mwaka 1389.Kabla ya hapo MTU yeyote aliebatizwa ndani ya Ukatoliki kwa sharti la jinsia ya kiume angeweza kuwa papa.
Papa kama kiongozi mkuu wa kanisa ana wajibu wa kuwateua Maaskofu na kuwapandisha vyeo kuwa makadinali na pia ana uwezo wa kufuta /kumfuta Mtumishi wa kanisa kwa kwenda kinyume na taratibu za kanisa kama alivyofutwa cheo cha Upadre,padre Privatus Karugendo wa jimbo kuu Rulenge.
Kwa taratibu za majina(Pontifical name).Kabla ya kuwa Papa kila Cadinali huwa na majina yake lakini siku akila kiapo hulazimika Kuchagua jina kutoka kwenye kitabu cha majina ya Upapa(papal name),kitabu hiki mpaka sasa kina jumla ya majina 83.
LENGO.
Wengi huchukua majina haya kama kutaka kurithi tabia za watangulizi wao.Kwa mfano Papa Benedict wa XVI alichukua jina ili kwa kumfuata mtangulizi wake yaani Papa Benedict wa XV aliengoza kanisa kwa miaka 7.5 na huku Benedict wa XVI akijiuzulu baada ya kuliongoza kanisa kwa miaka 8.
UTARATIBU. Kwa mujibu wa KANISA utaratibu huu ulianza  mwaka 533 AD baada ya mungu aitwaye Mercury kuchukua jina la John II kutoka kwa mtangulizi wake John I aliekuwa mtakatifu.Pia kuna Papa aitwaye MARCELLUS II mwaka 1555 alijipa jina lake mwenyewe..
Mwaka 1978 kadinali Albino Luciani alikuwa papa wa kwanza kuwa na majina mawili ,alifanya hivyo kama heshima ya watangulizi wake.Kwa mujibu wa kitabu cha majina ya Upapa majina yafuatayo ndio yanaongoza kwa kuchaguliwa:
1.John × 21
2.Gregory ×16
3.Benedict ×15
4.Clement ×14
5.Innocent ×13
6.Leo×13
7.Piu×12
8.Stephen ×9
KAULI ZA KANISA.
Kanisa Katoliki limesimamia kauli ya kwamba ni KANISA takatifu na la kitume na dini moja na imani moja ya kweli. KANISA hutoa Sakramenti 7 .Moja ya sakramenti ni ya ndoa ambayo ikifungwa ni mkatale hakuna kuivunja mpaka kifo.
Kauli ya KANISA kuhusu mapenzi ya jinsia moja.
Papa Francis mwaka 2013 akihojiwa na mwandishi wa habari kuhusu msimamo wa KANISA alisema"nadhani ni vigumu kumshambulia MTU moja kwa moja kwasababu hayo ni mambo binafsi,unawezaje kuweka utofauti kati ya MTU shoga na mwizi? Yote sio mambo mazuri. Kama MTU ni shoga na anamtafuta Bwana na ana nia nzuri, Mimi ni nani mpaka ni hukumu?

KUHUSU BIKRA MARIA.
KANISA Katoliki linamtaja mama huyu kwa kigiriki(Theotokos) yaani "mama wa Mungu". Mama Maria anaheshimiwa sana ndani ya Ukatoliki ambapo wengi wa waumini humtumia kama mbeba maombi yao kwenda kwa MUNGU.
KUHUSU MAUTI NA MAISHA YA BAADAYE
Kanisa Katoliki linataja sehemu tatu ambazo MTU akifa basi nafsi yake ufika
1.Mbinguni.Kanisa linataja watu ambao hawakuwa na dhambi katika maisha yao duniani kwamba huenda kwa Mungu baba mbinguni pia ni kwa mujibu wa Nicene creed.
2.Purgatory. Kanisa linaitaja kama sehemu ya kumaliza dhambi ndogo ,MTU alizokuwa nazo duniani. Sehemu hii ni ya mateso na baada ya dhambi kuisha basi roho huamia mbinguni.
3.Motoni.Kanisa linahitaja sehemu ya mashetani au watenda dhambi ambao watachomwa moto.Kwa mujibu wa dini ya wabudha wanaitaja kama" hell" wakiwa na maana ya sehemu sawa yenye Joto na baridi sawa.Hii ni kwa mujibu pia wa masharki ya Kati ila kwa Africa sehemu hii huitwa"kuzimu" yaani sehemu ya Giza.

Mtazamo wa wanazuoni.
Wengi wa wabobezi katika nyanja mbalimbali kama hisabati,sanaa,unajimu,sayansi na nyingine wamekuwa sio wepesi wa kukubali tu mambo.Watu hawa "polymaths" huwa nao wanafanya tafiti kulidhia ukweli wa mambo.
Nicolas Copernicus mzaliwa wa ujerumani aliyeishi kwenye karne ya 16 alianzisha kile kiitwacho Copernicasm ,ambapo alijitwalia mahali pa John Kepler aliekuwa akitafiti kama kweli kuna dunia pekee yake?
Mwaka 1564 akazaliwa Muitaliano Galileo Galilee ,naye alikuja kukazia kwenye Copernicasm na kuongeza zaidi kwa kuangaza "Copernican helliocentrism". Galilee alifanya alifanya utafiti na kugundua si dunia pekee ilikuwepo Bali dunia ilikuwa miongoni mwaka sayari nyingi zilizokuwa katika mfumo wa jua.Naye akagundua sayari ya Jupiter na kuuambia ulimwengu kwamba dunia ilikuwa na mizunguko mitatu.Yaani 1.Mzunguko wa kila siku 2.Mzunguko wa mwaka mzima na 3.Mzunguko wa kujizungusha katika mhimili wake.
Mambo haya yote Kanisa Katoliki lilikuwa likiyakataa na kutishia hata kufunga baadhi ya watu waliyoyasambaza maana yalikuwa kinyume na mtazamo na maandishi yao.Galileo alikuwa ni mpiga chetezo kanisani,kwahio Kanisa lilimfukuza na kumuona muasi.
Papa Paul II ndio alikuwa wa kwanza kuamrisha Kanisa kuchapisha machapisho ya Copernicus ambayo yalikuja kuzalisha kalenda Julian tunayotumia mpaka Leo.
Kwanini Kanisa Katoliki lilikataa " Copernicus "
Sababu zinaweza kuwa nyingi lakini moja inaweza kuwa alichosema Elbert Einsten kwamba "dini zinajaza ujinga". KANISA lilikaririsha watu kuamini kwamba MUNGU ni mmoja ambaye akili zake ni nyingi hazichunguziki na kwamba ameiumba dunia tu,hakukuwepo la zaidi bali kuamini hivyo. Huwepo wa Watu kama Galilee ulilipa Kanisa moto Kwa kuamini Watu wataliama Kanisa na kweli ndio Uprotestant ulikuja baada ya Kanisa Katoliki kukubali kuchapisha maandishi ya Copernicus.
Wanazuoni kama Nicolas Copernicus, Galileo Galilee, Johannes Kepler, Isaac Newton, Elbert Einstein mpaka kufika kizazi cha hakina Stephen Hawking ndio wameleta kitu kinachoitwa sayansi ya kisasa ya kuhoji na kuchunguza mambo.Aliwahi kusema Alberto Batistuta" mwanadamu anaweza kufanya kila jambo iwapo atapenda kufanya ".

TAKWIMU ZA KANISA
Kanisa Katoliki lina waamini waliobatizwa bilioni 1.3,Maaskofu 5237,Makasisi 415656,Watawa 45255 na Parokia 221700 hii ni kwa mujibu wa takwimu za Kanisa mwaka 2016.

_______***_______


Comments