Siku moja nilikuwa naongea na mwalimu ,Dr Bonephace kuhusu "ujauzito ni ugonjwa?". Swali ili lilikuwa linanipa wakati mgumu kwasababu moja ya tabia ya ugonjwa ni " dalili ".Ila kama mhudumu wa Afya ni rahisi kusikia MTU akikwambia" Nina ugonjwa wa homa " ni kawaida lakini ukweli ni kwamba hakuna ugonjwa wa Homa,bali io ni dalili ya ugonjwa.
Sasa dalili za ujauzito zimegawanyika katika makundi makuu mawili. Moja ni Dalili ya Uhakika na ya pili ni dalili ya Uwezekano.
1.DALILI ZA UWEZEKANO
Hizi ni dalili ambazo ni za awali kwenye ujauzito lakini huwa si za moja kwa moja kuthibitisha kama ni kweli kuna ujauzito isipokuwa Kwa vipimo .
Dalili hizi ni kama,
¶Ukosefu wa hedhi.Hii hutokea tu mimba ikitungwa.Sababu nyingine zinazoweza pia kusababisha Hii hali ni pamoja na Safari,uchovu,mifadhaiko,woga wa kupata mimba,matatizo ya homoni,ugonjwa,uzito kuongezeka au kupungua sana ,kunyonyesha.
¶Maradhi ya kila asubuhi(kichefuchefu,kutapika,).Hii huwa inatokea tu wiki ya 2 mpaka 8 baada ya mimba kutungwa.Ila kuna sababu zinazoweza pia kusababisha Hii hali kama kula chakula chenye sumu,mifadhaiko,maambukizi,na magonjwa mbalimbali.
¶Frequent urination.Hii hutokea tu mimba inapotungwa ndani ya wiki 2 mpaka 3.Sababu nyingine zinazoweza pia kusababisha Hii hali ni maambukizi kwenye mrija wa mkojo(uti),mifadhaiko,ugonjwa wa kisukari.
¶Sehemu ya mbele ya maziwa(areola) kuonekana nyeusi.Hii huwa inatokea tu kipindi cha awali cha ujauzito. Pia ina sababishwa na Matatizo ya homoni au matokeo ya ujauzito uliopita.
¶Kuchukia baadhi ya vyakula.Kipindi cha awali cha ujauzito hii hali ndio hutokea hasa miezi 4 ya awali.Pia sababu hii inaweza kusababishwa na lishe duni,mifadhaiko, na kukoma Kwa hedhi.
¶Michirizi ya bluu na pink kwenye maziwa mpaka tumboni.Hii hutokea kipindi cha awali cha ujauzito. Sababu za hali hii zinaweza kutokana na Matatizo ya homoni au ujauzito uliotangulia.
¶Mabadiliko ya uke kutoa maji maji ya bluu.Hii hutokea kipindi cha awali cha ujauzito. Pia hii inaweza kusababishwa na kukoma Kwa ujauzito.
.
¶Tumbo kuwa kubwa.Hii unaweza kuiona juma la 6.Hali kama hii inaweza
kusababishwa pia na uvimbe tumboni.
¶Dalili za kichanga kuzunguka tumboni .Hii huwa inatokea au unaweza kuhisi hali hii kuanzia wiki ya 16-22 ya ujauzito. Pia hii inaweza kusababishwa na gas tumboni au mapigo tu tumbo.
2.Sasa,tuone Dalili ambazo ni za UHAKIKA, nazo ni:
¶Matumizi ya Ultrasound kuangalia kichanga
Hii hutokea tu kipindi cha kati ya wiki ya 4 mpaka ya 6.
¶Mapigo ya kichanga .Hii ni kuanzia wiki ya 10-20 ya ujauzito
Dalili za ujauzito zinachunguzwa Kwa vifaa maalum kama Ultrasound na Doppler ili kuthibitisha ni ujauzito kweli au ni dhania kama tulivyoona hapo juu.Usije kuona Tumbo kubwa ukadhani io mimba,hapana inaweza kuwa ni kidonda kama nilivyosema.
YouTube
Comments
Post a Comment