Congo ni miongoni mwa nchi ambazo zina watu wenye vipaji vikubwa vya hasa kandanda na mziki.
Zaire ni ya kipindi cha Wabeligiji na Wafaransa lakini baada ya Kuingia Mobutu ilibadilishwa jina na kuitwa Democratic Republic of Congo (DRC).
Wakongo hupenda kuiita Zaire ya bankoko(Zaire ya Mababu).
ilikuwa
Mziki
Kitovu cha mziki hasa kwa Africa naweza kuthubutu kusema ni Congo na kanda yake nzima ya Afrika ya kati.Wakongo wana Rhumba,sebene,Sokous na mengi.
Congo Kwa ujumla imekuwa na majina ya wanamziki mashuhuri ndani ya Congo, Africa na nje ya Africa.Majina ya wanamziki kama Franco Luambo,Papa Wemba,Tabu Lei, Madilu system na wengine wengi.Moja ya Sifa ya vizazi kuendelea kuwa na mastaa wa mziki ni pamoja na wanamziki wakubwa kuwainua underground. Sam Mangwana anakiri swala ili alipokuwa akiojiwa na kusema "Madilu system" alikuwa ni dobi na kijana wa kazi za ndani nyumbani kwake,ambapo baada ya kumsikia akiimba mara kwa mara na sauti nzuri aliamua kumpeleka kwa Luambo Makiadi aliyekuwa kiongozi wa bendi ya TP OK jazz.
Leo tuangalie wanamziki wakubwa hawa watatu na mwendelezo wa kuinua Underground.
PAPA WEMBA
Ni jina la kisanii au la jukwaa lakini jina lake ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba mzaliwa wa Matonge. Papa Wemba aliezaliwa 14 June 1949 na kufariki 24 April 2016 baada ya kuanguka akiwa jukwaa ni ni mmoja wa Icon za mziki wa Congo. Papa Wemba ni zao la Band ya Zaiko Langa Langa. Maana ya Zaiko Langa Langa ni "Zaire ya maajabu" hii ni kwa mujibu wa Anuani ya Zaiko Langa Langa.
Ndani ya Zaiko Langa Langa ,Wemba aliingia mwanzoni mwa 1960 na Band hii ilikuwa na wanamziki kama Mavuela Somo,Evoloko Lay Lay,Teddy Sukami,Oncle Bapius,Zamuanganale Meneur,Manuaku Waku na N'yoka Longo.Kwenye bendi hii waimbaji walikuwa ni Evoloko "Lay Lay" joker,Papa Wemba,Gona Efonge,Mavuela Somo,N'yoka longo,Bimi ombale.
Na hawa ndio waanzilishi wa neno la Kavasha ambalo huwa tunalisikia.Mwanzilishi wa neno hili ni Meridjo Belobi alietaka ibuniwe radha au mapigo mapya ya mziki wenye sauti kama ya Garimoshi.Yeye alisema cavasha ikiwa na maana ya MACHINI YA KAUKA kwa kilingara yaani (Ingini ya garimoshi),mtindo wa kavasha uliendelezwa na bend ya Orchestra Shama shama miaka ya 1970.
Baadaye bendi hii iligawanyika ,ambapo Papa Wemba alienda kuanzisha bend yake ya Isifi Lokole akiwa na waimbaji kama Evoloko Ahsuamo,Mavuela somo huku Bozi Boziana nae akiwa anaimba Choral Mukoko alikuwa kwenye gitaa Djomali akiwa kwenye gitaa la Bass na Otis Koyongonda akiwa kwenye ngoma ya Lokole.Hii ilikuwa mwaka 1974,baadaye bendi ikavurugika ,basi Papa Wemba akaanzisha bendi ya Yoka Lokole mwaka 1975-1978 .Yoka Lokole ni kilingala chenye maana ya (sikia mbiu),Lokole ilikuwa ni ngoma ya zamani ya Zaire iliotumika kuashiria tukio kutokea.
Mwaka 1977 wakati CCM inazaliwa na pia Fall Ipupa alikuwa anazaliwa na ndio mwaka Papa Wemba alianzisha bendi ya Viva la musica.Bendi Hii ilikuwa na malengo ya kutafuta vijana wenye vipaji vya mziki na kwenye kutafuta wakapatikana vijana kam Kisangani Esperant ,Jadot Sombele,Pepe Bipoli,Petit Aziza,Lester Emeneya,Antoine Agbepa ,Bongo wende,Rigo star na Syrian.
Hapa anaonekana kijana mwimbaji na mtunzi Antoine Agbepa(Koffi olomide).Papa Wemba alikuwa akimtaja kijana huyu '"ooh I' homme idee) yaani "MTU wa madini"
........Basi safari ya Charles Koffi ikaanza.
KOFFI OLOMIDE
HILI ni jina la jukwaa ,yeye ni Antoine Christophe Agbepa Mumba aliezaliwa July 13 1956 Kinshasa. Mama yake alimuita Koffi kwa sababu alizaliwa Ijumaa.Mama yake ni Mghana na baba yake ni Mkongo.Koffi ni mbobezi wa masuala ya biashara na uchumi akiwa na Shahada ya uzamivu kutoka chuo cha Bordeaux na Shahada ya uzamili ya mahesabu kutoka chuo kikuu cha Paris Ufaransa. Waliosoma nae wanasema "jamaa ni kichwa".
Koffi Olomide carrier yake ya Mziki ilianzia Viva la Musica lakini mwaka 1986 alianzisha bendi yake inaitwa Quarter Latin International.Ndani ya Bendi yake kulikuwa na kuna wanamziki kama Fele Mudogo, Sam Tshintu,Suzuki 4×4,Cindy Le Coeur,Deo Brando,Fally Ipupa,Gibson Butukondee,Montana Kamenga,Soleile Wangapi na Bouro Mpela.
Koffi ameshinda tuzo nyingi ikiwepo ya msanii wa mlango(decade artist) yaani KORA.
Mwaka 2011 msanii Fally Ipupa alitoka kwenye bendi ingawa sababu hazijulikani ni zipi zilimtoa.
FALLY IPUPA
Ni jina kubwa Africa na duniani kote si mwingine ni Faustin Ipupa N'simba.Aliezaliwa 14 desemba 1977.Alianza kuimba akiwa kwenye Kanisa Katoliki mjini Kinshasa mwanzoni mwa miaka ya 1990.Safari nzuri ya mziki iliyomuweka kwenye ramani ilianza mwaka 1996 baada ya kuchukuliwa na kundi la Quartier Latin international chini ya Koffi Olomide.
Fally Ipupa amefanya kolabo na wasanii wa kubwa kama Youssou N'Dour,Salif Keita,Icha Kavons,2face Idibia,Lokua kanzi,Barbara Kanam,Olivia G-unit na WENGINE wengi.Ameshinda tuzo nyingi na za maana.
Kama ulivyo kwa " Zaire ya bankoko" natamani Naye Ipupa, X3 hustler,Di caprio marvelle ,love champions nae atupe mwanamziki kutoka kwenye bendi yake.
Tusubili labda tutaona.
______****_____
smart
ReplyDelete