Kucheza wasichana kwenye baadhi ya makabila mengi ni utamaduni wa jamii nyingi.
Kumcheza binti hakuna tofauti sana na ukeketaji maana zote ni tamaduni za unyago.Baadhi ya mikoa ambayo ni vinara wa shughuli hizi ni hasa mikoa ya ukanda wa Pwani .
Ni ipi tofauti ya ukeketaji na uchezaji wa msichana?
Kama jinsi ulivyo utaratibu wa unyago ,mambo mengi huwa ni ya siri sana na hata ukikutana na wahusika sio rahisi kukueleza mambo yao.
Katika mahojiano na kituo cha radio Capital FM ya jiji Dar es salaam bibi Nyamburi mkaazi wa Mugumu Serengeti anasema "huwa tunawakeketa watoto wa kike ili wakiolewa waweze kutulia ndani ya ndoa". Utaratibu wa ukeketaji huwa ni kwa watoto wa kike ambao hawajavunja ungo .Utaratibu ambao ni wa siri ambao huusisha mkeketaji na wazazi wa binti. Dada Fatima(sio jina lake halisi) ananiambia yeye wakati anapelekwa kukeketwa alikuwa darasa la pili kijiji kwao ,ambapo Shangazi yake alimchukua akidai anampeleka kumnunulia nguo na walimpeleka kijiji cha mbali mkoa wa Singida ambapo alifanyiwa kitendo hicho.Fatima aliniambia haya huku akitwokwa na machozi.
Tofauti ya kumcheza msichana na kumkeketa ni kwamba kumcheza msichana hakuondoi kiungo cha mwili.
Wengi wanaokeketwa wamekuwa si huru tena hasa wakiolewa na wanaume ambao si wa jamii io.Wengi wa wanaume katika Visa vingi vya ndoa kuvunjika,wanasema wanawake waliokeketwa hawana hisia za kufanya mapenzi labda hufanya kuridhisha wanaume tu. Kijana Daudi(sio jina lake) mkaazi wa Arusha anasema" nilipolala nae aliniuliza umemaliza?,kitu ambacho kilinishangaza na kuamua kumchunguza".
Wazaramo na kucheza wasichana.
Kabila hili ambalo lina takribani watu 1,238,000 na wengi wa Wazaramo ni wa dini ya kiislamu takribani 95.00% na huku Wakristo wakiwa ni 3.00%.Kabila hili linapatikana ukanda wa pwani hasa mkoa wa Dar es salaam.
Wazaramo akizaliwa binti huwa wanasherekea sana Kwa kuimba na kucheza ngoma zao za asili kama Mnanda na Chiriku.
Wazaramo pamoja na mambo yote wamekuwa wahanga wa kile kiitwacho "uswahili".Uswahili Kwa maana ya kuwa wa mambo yasiyo ya staha.Mzee Omar anasema Mwanamke wa kizaramo yuko radhi ndoa ivunje lakini audhurie shughuli ya kumcheza mtoto wa ndugu yake. Na hapa ndipo kikawa kichwa cha WAZARAMO NA MILA ZA KUCHEZA WASICHANA.
UTARATIBU.
shughuli nzima za kumcheza msichana huanza hasa kwa wasichana ambao wamevunja ungo.Wasichana hawa upelekwa kwenye nyumba maalum na huko hukutana na KUNGWI.Mtu huyu maalum huwa anafundisha taratibu nzima za unyumba na mambo ya ugoni nk.
Wasichana huambiwa mambo yote ya kiutu uzima kama Namna ya kumshika mwanaume kitandi,namna ya kumfikisha haraka kileleni(tafsida),namna ya kumtawala mwanaume, dawa za kuvutia mwanaume,dawa za kutoachika,kumiliki wanaume watu na zaidi (mafiga matatu) na mambo ya mikao wakati wa tendo la ngono wengi huiita kuzunguka na chupa.KUNGWI anaweza kuwa MTU wa makamo ambaye anafundisha taratibu zote Kutokana na uzoefu wake.MTU mmoja aliniambia Mwanamke wa kizaramo mpaka atulie labda wa miaka 50.
Kumcheza binti hakupo tu kwa WAZARAMO hata Mtwara,Zanzibar, Lindi haya mambo yapo.Naambiwa hukitaka kugombana na mkeo anaetoka kwenye makabila haya basi kataa mtoto wake kuchezwa.Kwanza, kwake anakuona mjinga usiejua chochote. Nadhani kuna vitu wanapata zaidi ya nilivyovitaja.
Baada ya binti kutoka huko uja akiwa tayari na anaweza kuozeshwa,wao huamini ni Mwanamke kamili.
Shughuli hizi hufanyika hasa mwezi wa sita (June) na Desemba wakati wa likizo.
Mambo ya pwani.
Comments
Post a Comment